LEICESTER CITY NA TOTTENHAM HAWANA MPINZANI ENGLAND
Na Albogast Benjamin
Kocha wa timu ya Leicester City Claudio Ranieri na mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane wameibuka vinara kwenye tuzo za EPL mwezi machi.
Ranieri ameiwezesha timu yake kuibuka na ushindi katika mechi tatu na kutoa sare mchezo mmoja hivyo kuifanya timu yake iendelee kushika nafasi ya kwanza akiwa na alama 69.
Naye mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane amefunga mabao 6 ndani ya mwezi machi na kuisadia timu yake ya Spurs kukaa kwenye nafasi ya pili.
Kocha Claudio Raniel amechukua tuzo hii kwa mara ya pili ndani ya msimu huu. Kwa upande wa Kane yeye mpaka sasa anaongoza kwa wafungaji wa mabao ligi ya Engaland akiwa na mabao 22.