Na Amini Nyaungo
Viporo muda mwingine vinaweza kuharibika ila muda mwingine hata kikichacha unakipasha na kukila tena maisha yakasogea ukapata uhai.
Yanga Africans wameweza kupata ushindi dhidi ya Kagera Sugar katika kiporo chake katika Ratiba iliyo pangwa upya na Tff,Kagera ndio walikuwa wa kwanza kupata goli dk ya 8 mfungaji akiwa Mbaraka Yusufu kabla ya Yanga kurudisha dk ya 20 kupitia kwa Donald Ngoma.
kipindi cha pili kilipo anza mchezaji Shabaan Ibrahim wa Kagera alipata kadi ya pili ya njano na kutolewa nje kwa kadi nyekundu. dk ya 63 Amis Tambwe akapeleka kilio Kagera alipoweka goli lake la 18 msimu huu wakati Mwinyi Haji akiunganisha kwa kichwa kona na kufanya matokeo Yanga 3 Kagera 1 hadi kipyenga cha mwamuzi kina pulizwa kuashiria mwisho wa mchezo.
Wakati huo huo Azam wanashindwa kula kiporo kilicho chacha ugenini baada ya kulazimisha sare ya goli 1-1 dhidi ya Toto Afrika Goli la Azam lilifungwa na John Boko dk ya 23 kabla ya Waziri Juma kurudisha kiporo jalalani dk ya 40. Azam 1 Toto 1.
Matokeo haya yanazidi kufanya mchuano wa kumpta bingwa kuwa mgumu sana ambapo sasa Simba amesalia kileleni akiwa na alama 57 Yanga akiwa nafasi ya pili na alama 53 huku Azam akibaki nafasi ya tatu na pointi 51.