Our Feeds

Sunday, 3 April 2016

Unknown

WACHEZAJI EPL KWENYE SKENDO KUBWA YA MATUMIZI YA DAWA ZA KUONGEZA NGUVU

Na Albogast Benjamin
Serikali ya Uingereza imeanzisha uchunguzi wa dharura kufuatia ufichuzi kuwa wachezaji nyota wa kandanda nchini Uingereza wamekuwa wakitumia madawa yaliyopigwa marufuku ya kuongeza nguvu mwilini.
Gazeti la Sunday Times limechapisha ripoti ya uchunguzi iliyothibitisha kuwa sio tu wasakataji dimba bali hata waendesha baiskeli, wachezaji Kriketi na hata wachezaji wa tenisi wamekuwa wakipokea matibabu kutoka kwa daktari mmoja ambaye anajulikana kwa kupeana madawa hayo yaliyopigwa marufuku ya kututumua misuli.
Daktari Mark Bonar ambaye anazahanati yake mjini London Uingereza amekuwa akiwatoza wachezaji nyota maelfu ya pauni za Uingereza kwa matibabu hayo siri ambayo imegunduliwa kuwa ni matibabu ya madawa yaliyopigwa marufuku na shirikisho la kupambana na madawa haramu WADA.
Uchunguzi pia umebaini kuwa dkt Bonar amekuwa akiwapa wachezaji nyota 150 dawa aina ya EPO Steroids inayosisimua misuli kwa miaka 6 sasa.Aidha Sunday Times linasema kuwa halina ushahidi 'huru' kuwa dkt Bonar aliwapa madawa hayo ya kututumua misuli wachezaji wangapi wanaochezea vilabu vya ligi kuu ya Uingereza EPL.
Hata hivyo wachezaji kadhaa walioulizwa iwapo walipewa madawa hayo ya kututumua misuli na dkt Bonar walikataa kujibu na wengine wakakanusha madai hayo ya daktari huyo.Uchunguzi huu unatokana na ufichuzi wa mchezaji mmoja aliyekwenda kwa idara ya serikali kumshtaki dkt Bonar kwa kumpa dawa iliyopigwa marufuku.
Credit: BBCSWAHILI

Subscribe to Mtembezi Sports via Email :
Previous
Next Post »