Na Albogast Benjamin
Leicester City imezidi kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi ya England kwa pointi 7 zaidi ya Tottenham wanaoshika nafasi ya pili baada ya jana kulazimishwa sare na Liverpool na kuwafanya Leicester wapanue wigo wa pointi wakati huu ambapo zimebaki mechi sita ligi ifike tamati.
The foxes kama wanavyojulikana walipata bao kipindi cha kwanza baada ya kazi nzuri ya nahodha wao Christian Fuchs kumaliziwa na Wes Morgan na kufanya vijana hao wa Kings Power waongoze hadi mwisho wa mchezo wakichagizwa na mashabiki waliopewa bia na donati kabla ya mechi kuanza na mmiliki wa klabu hiyo aliyekuwepo leo uwanjani kwaajili ya maandalizi ya siku yake ya kuzaliwa hapo kesho.
Southampton walikosa mara kadhaa kupitia kwa Sadio Mane akishirikiana na Kasper Schmeichel, lakini mpira uliokuwa unaelekea golini uliokolewa na Danny Simpson. Leicester City sasa rasmi wanayo nafasi ya kuchukua ubingwa wa EPL endapo tu watshinda michezo yao minne kati ya sita iliyosalia.Vijana hao wa kocha Claudio Ranieri wameshinda michezo yao mitano kati ya sita iliyopita.
Msimamo wa EPL sasa unaonyesha nafasi tatu za juu zinaongozwa na Leicester City akiwa na pointi 69 baada ya michezo 32, Nafasi ya pili yupo Tottenham akiwa na alama 62 na michezo 32, Arsenal ikiwa namba 3 na alama 58 baada ya michezo 31, Nafsi ya 4 Manchester City akiwa na alama 54 na michezo 31. Mchezo unaoendelea hivi sasa ni kati ya Manchester United dhidi ya Everton na bado hawajafungana kipindi cha pili.