Our Feeds

Wednesday, 13 April 2016

Unknown

BOSS WA SOKA LA ZANZIBAR KUPATIKANA KESHO



Na Martha Magawa

Kinyang'anyiro cha kuwania nafasi tatu za juu za Chama Cha Soka Zanzibar ZFA, kitajulikana baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa chama hicho, uchaguzi huo utakaofanyika kesho saa nne za asubuhi katika uwanja wa Gombani, huku ukiwa chini ya ulinzi mkali wa askari Polisi, Mgeni Rasmi akitarajiwa kuwa Mkuu wa wilaya ya Chake Chake Mhe:Hanuna Ibrahim Masoud.

Uchaguzi huo ambao wajumbe 60 wa mkutano mkuu wa ZFA Zanzibar, wataweza kuchagua Rais na makamo wake wawili ambao ndio watendaji
wakuu wa Chama hicho.

Jumla ya wagombea wawili wameweza kujitokeza katika kuwania nafasi hiyo ya uras akiwemo Rais aliyepo Madarakani, Ravia Idarous Faina, huku akikabiliwa na upinzania mkali kutoka kwa Kocha Salum Bausi.

Nafasi ya Makamo wa Rais wa ZFA Taifa Pemba Ali Mohamed Ali akichuwana na Suwedi Hamad Makame, huku Upande wa Uguja wanaogombania nafasi ya Makamo ambayo imewachwa wazi na Haji Ameir Haji, aliyevuliwa nafasi hiyo na wajumbe wa mkutano mkuu wa ZFA, ikigombaniwa na Mohamed Massoud Rashid, Ali Salum Nassor na Mzee Zam Ali.

Akizungumza mtembezi juu ya maandalizi ya Uchaguzi huo Makamo wa ZFA Taifa Pemba Ali Mohamed Ali, alisema maandalaizi yote ya Uchaguzi huo yameshakamilika, ikiwemo kwa wajumbe kutoka unguja kuwasili Pemba pamoja na waandishi wa habari za michezo Unguja.

Subscribe to Mtembezi Sports via Email :
Previous
Next Post »