Our Feeds

Wednesday, 13 April 2016

Unknown

ROBO FAINALI UEFA LEO NI MWENDO WA KAMPA KAMPA TENA


Na Albogast Benjamin 

Ifikapo saa tatu na dakika arobaini na tano usiku 9:45, utakuwa ni muda wa wapenda soka kuelekeza macho yao pale kwenye dimba la Vicente Calderon nyumbani kwa Atletico Madrid, kwenye mchezo wa robo fainali mkondo wa pili ambayo ni kumbukumbu tosha ya msimu wa 2014 ambapo Barcelona waliaga katika hatua hiyo na kuwaacha Atletico wakitinga hadi hatua ya fainali.

Vikosi vya msimu huo:

Atlético:  Courtois, Juanfran, Godín, Miranda, Filipe Luís, Gabi, Tiago, Koke, Adrián López (Diego 62), Raúl García, Villa (Rodríguez 79).
Barcelona:  Pinto, Alves, Bartra, Mascherano, Alba, Xavi, Busquets, Iniesta (Pedro 72), Fàbregas (Alexis Sánchez 61), Messi, Neymar.
Mchezo huo uliamuliwa na goli pekee la Koke dakika ya 50 na kuharibu rekodi ya Barcelona ya kufika nusu fainali misimu sita mfululizo.

Mchezo wa leo:
Wiki moja iliyopita timu hizi zilicheza pale Camp Nou na matokeo yalikuwa ni 2 kwa Barca na 1 kwa Atletico, Mchezo wa leo unategemewa kuwa na ushindani wa hali ya juu ambapo kila timu inayo nafasi ya kusonga mbele ukizingatia Atletico wanahitaji bao moja tu huku Barcelona wakitafuta sare yoyote ili wasonge mbele. Mwamuzi Nicola Rizzoli ndiye ataamua dakika 90 za pambano hilo.


Mchezo mwingine:

Mchezo mwingine usiku wa leo utapigwa nchini ureno kati ya Benfica  na Bayern baada ya mchezo wa kwanza uliofanyika Alianz Arena kumalizika kwa Bayern kushinda bao moja. Benfica ambayo inaonekana kurejea kwenye ubora wake kama ule wa mwaka 2006 ilipokutana na Barcelona kwenye robo fainali itakuwa inasaka tiketi ya nusu fainali mbele ya kikosi cha Bayern ambacho kinafundishwa na kocha Pep Guardiola na ndoto yake kubwa ni kubeba taji hili kabla hajatua Manchester City msimu ujao.

Subscribe to Mtembezi Sports via Email :
Previous
Next Post »