Na Albogast Benjamin
Kocha wa timu ya taifa ya Italy Antonio Conte ametangazwa rasmi kuwa mrithi wa Mourinho ndani ya klabu ya Chelsea.
Timu hiyo imethibitisha jumatatu hii kuwa wamesaini mkataba wa miaka mitatu na kocha huyo mwenye umri wa miaka 46.
Conte ataanza kazi rasmi mwezi Julai mwaka huu akitokea Ufaransa kwenye mashindano ya Euro 2016 yanayotarajiwa kufanyika kuanzia June 10 hadi July 10.
Kocha huyo atachukua nafasi kwenye klabu hiyo baada ya kutimuliwa kocha Mourinho ambaye alipokelewa na kocha wa muda Guus Hiddink anayetarajia kuachia ngazi baada ya ligi kumalizika.
Je? ujio wa Antonio Conte ndani ya Chelsea utakua na tija hasa kipindi hiki ambacho Hazard anawaza kwenda vilabu kama PSG na Madrid tena ndio muda ambao Willian anatamani kuwepo kwenye vilabu vyenye uhakika wa kutwaa mataji makubwa na muda huo huo Fabregas anaonekana kama ameanza kupisha njia wakati Diego Costa mpira umegoma miguuni kageuka mbogo kwa wapinzani.
Makocha wengi wanaotoka kwenye timu za taifa hadi kwenye soka la vilabu inawawia vigumu sana kuweza kufanya vizuri mfano mzuri ni kwa kocha wa Manchester United ambaye alikuwa anafanya vizuri na timu ya taifa ya Uholanzi lakini bado hajawa na msimu mzuri.