Our Feeds

Monday, 4 April 2016

Unknown

NOVAK DJOKOVIC ATWAA UBINGWA WA 63 MIAMI OPEN


Na Albogast Benjamin
Unamjua vizuri nyota namba moja kwa ubora wa mchezo wa tenesi duniani kwa wanaume?
Si mwingine ni Novack Djokovic ambaye ameendelea kutamba katika mchezo huo kwa kuongeza makombe ya ubingwa kwenye kabati lake usiku wa kuamkia leo.
Djokovic ametwaa ubingwa wa michuano ya wazi ya Miami kwa kumshinda mpinzani wake Kei Nishikori, kwa kumchapa kwa jumla ya seti mbili kwa 6-3 6-3.
Ushindi huo unampa nyota huyu wa tenesi taji la 63 toka alivyoanza kucheza mchezo huu katika ngazi ya ushindani.
Sasa unapomwongelea Novak unakuwa umemaanisha Mchezaji aliyeingiza kiasi cha $1,028,300 baada ya mchezo huo na kwa sasa ndio anaongoza kwa wacheza tenesi wanaoingiza pesa nyingi akiwa amefikisha kiasi cha $100 million, katika muda aliocheza mchezo huo.

Subscribe to Mtembezi Sports via Email :
Previous
Next Post »