Our Feeds

Friday, 1 April 2016

Unknown

DI MARIA AFICHUA KILIMCHOMTOA MAN UNITED


Na Albogast Benjamin

Mchezaji wa Argentina na klabu ya Paris Saint Germain Angel Di Maria amesema ilimbidi aondoke Old Traford kutokana na kuchezeshwa nafasi tofauti na aliyozoea lakini pia hakupewa nafasi ya kutosha.

Amesema kuchezeshwa kwake nafasi asiyoifurahia ndio kitu kiichomwondoa pamoja na kwenda kutafuta nafasi ya kushinda makombe ambayo aliona akibakia Manchester United asingeweza kuyapata ikiwemo ubingwa wa Uefa.

Di Maria alikaa msimu mmoja ndani ya Uingereza ambao haukuwa na mafanikio kwake pamoja na kusajiliwa kwa dau kubwa kutoka Real Madrid.

Nyota huyo mwenye miaka 28 amekuwa na msaada mkubwa kwa klabu ya PSG ambapo ameisadia kuchukua ubingwa mapema msimu huu lakini pia akiwa ameisadia timu yake kufika hatua ya robo fainali ya Michuano ya Uefa baada ya kuitoa Chelsea.

Di Maria amesema kwasasa  anafuraha kuwa ndani ya PSG na anamatumaini kuwa watachukuwa kombe la Uefa msimu huu ili kutimiza ndoto yake hiyo.

Katika hatua nyingine mchezaji huyo amemtupia lawama kocha Van Gaal kwa kushindwa kuleta mabadiliko toka ameanza kuifundisha timu ya Manchestaer United msimu 2014/2015.

Subscribe to Mtembezi Sports via Email :
Previous
Next Post »