Na Amini Nyaungo
Faida ya kujitunza na kuwa na maadili katika kazi ni moja ya silaha muhimu sana ambayo itaweza kukuweka mchezaji katika mazingira mazuri, Tanzania tumewahi kuwaona wachezaji waliojitunza na kucheza kwa muda mrefu leo mtembezisports inamwanganzia mmoja wao alijulikana kama Mzee wa kiminyio.
Madaraka Suleiman mzee wa kiminyio kwa shabikia yeyote wa mpira na sok la Bongo huwezi kumsahahu fundi huyu tena ufundi wake ungekuwa ni leo maika ya kuona mojamoja michezo ya ligi basi huenda asingekuwa na maisha aliyonayo hapa naamanisha huenda angesogea Ulaya na angecheza bila shida yoyote kutokana na kuwa na umbo la mpira lenye mazoezi haswa, kikubwa zaidi Madaraka Suleiman alistaafu akiwa na miaka 40 na akiwa katika ubora wake.
KIPI KILIMPA UWEZO MADARAKA KUCHEZA KWA MUDA WOTE HUO?
Alijitunza,alijiheshimu, hakujiona star zaidi ya mwenzake zaidi na zaidi alizingatia mazoezi hivi vyote vilimfanya adumu kwa muda mrefu na hii ndio silaha muhimu kwa wa chezaji wa sasa sidhani kama kuna anaye weza kufika kule kwa Madaraka japo kila jambo linawezekana ukiweka nia na malengo.
KIPI KINA WASHINDA WACHEZAJI WA LEO?
Hapa hakuna muda wa kueleza sana wachezaji wa leo hawana nidhamu,wanajawa na sifa mapema,starehe na majivuno. Mpira hauendi hivi wengi watashindwa kufika kileleni kwa hivyo nilivyo eleza wakivirekebisha huenda tukapata Samatta na Thomas Ulimwengu wengine wengi na vipaji Tanzania vipo.
Mzee wa kiminyio alicheza na Nteze John Rungu,Machupa,Emanuel Gabriel na wengine lakini kwa pamoja walitengeneza timu imara iliyoweza kuzitoa timu kama Zanako na Zamaleki kwenye michuano ya kimataifa mwanzoni mwa miaka ya 2000.