Amini Nyaungo
Mshambuliaji wa Chelsea na timu ya taifa ya Hispania Diego Costa amekumbana na rungu la chama cha soka England FA kwa mara nyingine tena kufuatia kosa la tarehe 12 March Chelsea ilipokutana na Everton mchezaji huyo alipata kadi nyekundu kwa kosa la utovu wa nidhamu.
Hii imekuja baada ya mchezaji huyo kutokuwa na nidhamu ya mchezo kwenye mechi hiyo alipomtishia kumng'ata mchezaji Barry, Diego Costa atakosa mechi ya Swansea city na ile ya Aston Vila.
Costa ameongezewa adhabu hiyo pamoja na faini kwa kosa la kumfokea mwamuzi Michael Oliver pia alikataa kutoka nje ya uwanja baada ya kupewa kadi nyekundu. Costa amekuwa na msimu usio mzuri mwaka huu baada ya timu yake ya Chelsea kushindwa kufanya vizuri ikishika nafasi ya 10 huku ikiwa imetolewa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa.