Na Amini Nyaungo
Ladies and Gentlemen welcome Camp Nou Barcelona host Real Madrid to El Clasico 2015/2016. Hapo lazima mtangazaji umsikie kesho haswa mtangazaji wa England John Champion huwa anayatumia sana maneno haya kwenye EPL, kuelekea El Clasico Barcelona akimkaribisha Real Madrid katika dimba la Camp Nou.
JE WAJUA REKODI ZAO?
1. El Clasico ilianza pale tu ligi ya Hispania ilipoanzishwa 1929 Barcelona na Real Madrid miongoni mwa timu tatu hazikuwahi kukosa hata msimu mmoja tangu ligi hiyo ianzishwe ikiwemo Athletic Bilbao.
2. Hii itakuwa mara ya 231 wanakutana wakiwa tayari wamekutana mara 230 Real Madrid ameshinda mara 92 sawa na asilimia 40 huku Barcelona akishinda mara 90 sawa asilimia 39 wakitoka droo mara 48 sawa na asilimia 21.
3. Real Madrid imefunga magoli mengi 278 kuliko Barcelola ikifunga 272
4. Mara ya mwisho Barcelona imeshinda magoli 4-0 magoli ya Suarez akifunga mara 2 huku Neymar na Iniesta wakifunga bao moja kila mmoja kwenye dimba la Santiago Bernabeu.
5. Messi ndiye mchezaji anayeongoza kwa kufunga Elclasco akiwa amefunga mara 21.
7. Wachezaji waliocheza ElClasco nyingi ni Francisco Gento (Real), Manuel Sanchis Martinez (Real) and Xavi (Barcelona) with 42.
8. Ushindi mkubwa ulikuwa mwaka 1943 Real Madrid waliposhinda bao 11 kwa 1.
9. Wanakutana makocha ambao walishawahi kucheza katika timu hizo kwenye miaka ya 90 na mwanzoni mwa 2000 na walikuwa na ushindani wa hali ya juu uwanjani hivyo tusubiri kuona nani ataibuka mbabe.