Na Amin Amali
Ligi kuu ya Tanzania Bara imeendelea leo viwanja viwili vimewaka moto Coastal Union inaonekana jahazi kuzama kwani imekubali kichapo kutoka kwa wana wa jiji la Mbeya,ambapo Mbeya City imempa kichapo Coastal Union magoli 4-0
Hayo yakiendelea kule Shinyanga Mwadui imekubali kunywa maji ya miwa ya Mtibwa Sugar mabao 2 kwa 1.
Ligi hiyo inaendelea kesho Yanga atawakaribisha Kagera sugar wakati Azam atacheza watache na Toto Africans.
Katika hatua nyingine vijana wa Tanzania wenye chini ya umri wa miaka 17 wameichapa Misri mabao 2-1