Na Albogast Benjamin
Mchezo wa ligi kuu ya Hispania kati ya Barcelona na Real Madrid maarufu kama ELCLASCO ndio mchezo unaotazamwa na watu wengi zaidi duniani kwasasa kutokana na ushindani na ubora wa timu hizo, April 2 umechezwa tena na mara hii Madrid wameshinda mabao 2 kwa 1 na wamelipa kisasi cha kufungwa nyumbani kwenye mkondo wa kwanza.
Mmabo mhimu mawili yaliyoamua mchezo huo.
1. ZIDANE KAMA KOCHA AMEFANIKIWA KUBUNI MBINU YA KUCHEZA NA BARCELONA
Katika msimu wake wa kwanza tu miezi michache tangu achukue kibarua ameweza kuonyesha mabadiliko makubwa ya kiuchezaji alkini leo ameingia na mbinu moja tu ambayo inaweza kufanana na staili ya Mourinho lakini tofauti inakuja kwenye kumiliki mpira wakati timu inakwenda kushambulia.
Aliamua kuwekeza kwenye kujilinda na kujihami zaidi wakati huo anajua amemwacha mtu mmoja mbele ambaye ni Benzema huku akisaidiwa na winga wenye kasi Ronaldo na Bale na mara zote timu ya Madrid ilipokuwa na mpira wakijaribu kupiga pasi za haraka ili kuwafikia watu hao wa pembeni na alifanikiwa kuwazuia Barcelona akiwacha wamiliki mpira lakini yeye alikuwa anasumbiri kushambulia kwa kushitukiza na imempa matokeo Slute Boss Zizou.
2. MABADILIKO YA RAKITIC NA ARDA TURAN DAKIKA YA 73
Hapa Boss Enrique ndipo alipokosea kwenye mchezo wa leo na imesababisha apoteze mchezo kwenye uwanja wa nyumbani.
Iniesta hakuwa kwenye kiwango kizuri ukizingatia ametoka kwenye majeruhi hivyo kabla ya kumwingiza Arda Turan alitakiwa afikirie zaidi kwasababu Arda si mtu wa utamaduni wa kuchezea mpira na Barclona silaha yao kuu ni kumiliki mpira baada ya Rakitic kutoka mambo yakabadilika na Arda hakuonekana akigusa mpira zaidi ya mara tano ndani ya dk 17 alizocheza hapa utagundua jinsi Iniesta alikosa msaada na kuruhusu mashambulizi ya haraka kutoka kwa Madrid wakitumia kaunta attack na mwisho wakafanikiwa kupata bao la pili na wakamaliza mchezo.
Bao la Barcelona lilifungwa na Gerad Pique kwa kichwa kufuatia mpira wa kona ulipigwa na Rakitic dakika ya 56 kabla ya Benzema kuunganisha krosi ya Tony Kroos na kupachika bao la kusawazisha, Bao la ushindi lilifungwa na Cristiano Ronaldo alipopokea pasi ya Gareth Bale akatulia vizuri akaweka kifuani na kupiga Shuti la chini iliyompita tobo golikipa wa Barcelona Claudio Bravo.