Na Albogast Benjamin
Mechi ya leo kati ya Barcelona na Real Madrid inakutanisha pande mbili zenye safu ya ushambuliaji Ghali zaidi kuwahi kutokea kwenye historia ya soka wakati Barcelona wakiwa na MSN Real Madirid wan BBC kizuri zaidi wote wanategemewa kuanza kwenye mchezo wa leo.
Kivutio kikubwa kwenye mchezo huu kinaweza kisiwe ushindani wa ubingwa kutokana na Barcelona kuizidi Madrid alama 10 kwenye msimamo wa ligi ya La liga lakini dunia itakuwa imeketi kuangalia jinsi washambuliaji hawa MSN Lionel Messi, Luis Suarez na Neymar dhidi ya BBC Cristiano Ronaldo, Karim Benzema na Gareth Bale jinsi wanavyopambana kuchukua kiatu cha dhahabu msimu huu.
TUMTAZAME MMOJA BAADA YA MWINGINE NA NAFASI YA KUTWAA PICHICHI
CRISTIANO RONALDO (mabao 28 )
Ronaldo amecheza dakika zote kwenye mechi za ligi msimu huu na anaongoza kwa mabao hadi sasa akiwa amefumania nyavu mara 28.
Ronaldo hajafunga goli kwenye mechi dhidi ya wapinzani wao walioko kwenye nafasi nne za juu kwenye msimamo wa ligi msimu huu ambao ni Barcelona,Atletico na Vllareal
LUIS SUAREZ (mabao 26 )
Suarez ndiye anaongoza kwa mabao msimu huu kwenye mashindano yote ndani ya Barcelona akiwa na mbao 43 kwenye michezo 43
Kitendo cha Messi kumpa pasi ya penati Suarez kwenye mchezo na Celta Virgo pamoja na kumwachia apige penati kwenye mchezo dhidi ya Sporting Gijon vinatafsiriwa kama mbinu za kumfanya achukue kiatu kwa kumpiku Ronaldo lakini yote kwa yote huenda ni mbinu ya ushindi.
LIONEL MESSI (mabao 22 )
Messi hadi sasa amepachika mabao 22 pamoja na kuwa hakucheza miezi miwili akiwa majeruhi lakini toka amerejea amekuwa kwenye kiwango kizuri.
Messi atakuwa anatafuta bao lake la 500 kwenye maisha yake ya soka baada ya kufikisha bao 499 alipofunga bao moja kwenye timu yake ya taifa Argentina dhidi ya Bolivia na kufikisha mabao 50 kwenye timu ya taifa.
NEYMAR (mabao 21 )
Neymar amefunga mabao 4 kwenye mechi tatu za mwisho baada ya kutofunga kwenye mechi kadhaa baada ya Messi kurudi kutoka majeruhi, Mwezi October na November Neymar alifunga mabao 9 kwenye mechi 6 alizokosa Messi.
KARIM BENZEMA (mabao 20 )
Benzema akiwa na mabao 20 msimu huu amekuwa na wasitani wa kufunga kila dakika 78 za mchezo wa Laliga kila anapokuwa uwanjani hivyo naye yupo vizuri kwenye kufukuzia kiatu cha dhahabu.
GARETH BALE (mabao 15 )
Bale anakumbukwa vizuri kwenye mchezo wa ELCLASCO kutokana na bao lake mwaka 2014 kwenye fainali ya Copa del rey alipokimbia kutokea nje ya uwanja kwa kumzunguka beki wa Barcelona Bartra kisha akaenda kufunga na limekuwa bao lake la pekee kwenye Elclasco tangu atue Madrid. Msimu huu pia amekuwa nje kwa mechi kadhaa kutokana na majeraha.
Mchezo huu unatarajiwa kuchezwa badae saa 3 na dakika 30 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.