Our Feeds

Wednesday, 13 April 2016

Unknown

HAWA HAPA WANAUME WAWILI WA KWANZA KUTINGA NUSU FAINALI


Na Albogast Benjamin

Tumezoea kuona walinda mlango wakipanda kiwango kadiri miaka inavyoongezeka lakini mara hii imekuwa tofauti. Wakati golikipa wa Zamani wa Real Madrid Iker Casillas akishuka kiwango ndio Nyota wa timu hiyo Mreno Cristiano Ronaldo akipanda kiwango wakati umri nao unapanda ni adimu sana mchezaji kwenda sambamba na mambo haya mawili.

Wakati Chelsea ya Mourinho ikimwona si kitu si lolote winga Kelvin De Bruyge, Man City ilitambua kipaji chake na Kuamua kumrudisha England na kiwango chake kinapanda kila kukicha na  amekuwa msaada mkubwa kwa timu.

Najua utakuwa umeelewa nini nazungumzia ni "Usiku wa Ulaya" hatua ya robo fainali. Madrid wakicheza mbele ya mashabiki elfu80 kwenye uwanja wao wa Santiago walikuwa wakimtehemea mwanaume mmoja kutoka Ureno.

Kwenye Dimba la Etihad Man City wakiwa na shauku ya Kufuzu hatua ya nusu fainali kwa Mara ya kwanza wamepita kwa ushindi wa jumla ya mabao 3 - 2. Bao la Kelvin De Bruyge dakika ya 76 limeipa tiketi ya nusu fainali timu hiyo kufuatia sare ya 2 - 2 kule Ufaransa na kilichobaki ni kwa Ibrahimovic kupanda ndege kurudi jijini Paris au kubakia jijini Manchester ili kumalizana na Man United.


Cristiano Ronaldo alitumia dakika ya 15 na 17 za kipindi cha kwanza kusawazisha mabao 2 ya Wolfsburg kwenye mchezo wa kwanza kule Ujerumani. Kipindi cha pili alitumia dakika ya 77 kuipeleka Real Madrid nusu fainali ya Uefa wakati huo akiwa amepiga bao lake la tatu "Hart Trick" kwenye mchezo huo na la 17 kwenye michezo 10 ya Uefa msimu huu. 


Subscribe to Mtembezi Sports via Email :
Previous
Next Post »