Na Albogast Benjamin
Kocha wa Manchester United Louis Van Gaal amewaonya wachezaji wake kuwa makini na "Andy Carroll Show" mshambuliaji wa West ham kwenye mchezo wao wa jumatano hatua ya robo fainali kombe la FA.
Andy Carroll alipiga show ya dakika sita akipachika mabao matatu kwenye mchezo dhidi ya Arsenal wikiend iliyopita hivyo Van Gaal anahofia kutopoteza mechi yake hiyo ambayo inaweza kuwa nafasi ya pekee kutwaa ubingwa msimu huu kama atafanya vizuri.
"Niliona Andy Carroll show ( dhidi ya Arsenal) ," Mholanzi huyo aliwaambia waandishi wa habari . " Carroll ana sifa za ziada na tuliona hilo kwenye mechi na Arsenal."
Arsenal ina walinzi wazuri lakini tuliona Andy aliwafunga hivyo nasisi sehemu yetu ya ulinzi inabidi kuwa makini na mshambuliaji huyo.