Na Amini Nyaungo
Huenda kauli ya Kocha Jamhuri Kihwelo imekamilika kwani alisema dhahiri kuwa Anaomba Nusu fainali apangiwe na Azam ama Coastal Union ili akutane na Yanga Fainali.
Jamhuri ni kocha mwenye Radha ya maneno mengi mara nyingi hufananishwa na Jose Mourinho kwa Mbwembwe zake akiwa uwanjani lakini pia akizingumza huwa Watanzania wanafurahishwa na matamshi yake.
MAWAZO YAKE.
Endapo ataingia Fainali ya Michuano hiyo na huku Yanga nao wameingia katika michuano hiyo endapo Yanga wakichukua Ubingwa sheria ina ruhusu kuwa mshindi wa pili wa FA ashiriki Michuano ya Kombe la Shirikisho la soka Barani Afrika. kwa Mwaka huu Mshindi wa VPL na mshindi wa FA ndio watakaowakilisha nchi katika michuano ya kimataifa.
RATIBA YA NUSU FAINALI
YANGA VS COASTAL UNION
AZAM VS MWADUI