
HIKI KIKAO CHA WATU WAZIMA MTOTO KAA KANDO, MAN CITY Vs PSG
Na Amini Nyaungo
Ni kitendawili cha kuweka historia je Manchester City ama Paris Saint Germain kuweka historia ya kuingia Nusu Fainali ya michuano hii mikubwa ya Ulaya UEFA Champions league? Sare ya magoli 2-2 pale Park De Princes imebakia kuwa jipu ambalo jumanne saa 9:45 usiku ndipo mtanange huo utachezwa na jipu kutumbuliwa.
MUUNGANIKO WA VIUNGO WA PSG
Muunganiko wa Marco Verratti Thiago Mota na Blaise Matuidi katika kiungo cha PSG huu umeleta ubora sana katika timu hiyo haswa jinsi wanavyocheza kwa kuelewana mmoja akipanda wengine wanashuka pasi za uhakika na ukabaji makini, hakika 'couple'hii inafanana na ile bora kabisa ya Xavi Hernandez na Iniesta japo hawa wakina matuidi hawawezi kufika kama walivyo wakongwe hawa.
MAJERUHI
Kocha wa PSG Laurent Blanc anataka kumrudisha Verratti ili aje asaidie timu hiyo ambapo alipata majeraha siku za nyuma mchezo uliopita hakucheza inataarifiwa kuwa ataweza kuwepo japo alirudi katika mazoezi lakini umuhimu wake wataweza hata kumdunga sindano ili awasaidie kwani ilishafanyika hii kwa Wayne Rooney na wachezaji mbalimbali pindi walipohitajika kusaidia timu zao.
Manchester City itataka kupambana ili ijiwekee rekodi ya aina yake kuweza kufika hatua hiyo ya juu ambayo haijawahi kufika tangu ianze uwekezaji mkubwa imekuwa ikiishia mtoano au robo. Ripoti ya jana kuhusu Vincet Kompany kuanza mazoezi huenda ikakipa nguvu kikosi cha Peregrini ambacho kinakabiliwa na majeruhi kadhaa kama David Silva lakini kitakuwa na nguvu baada ya nyota wake Kelvin De Bruyge kurejea.