Our Feeds

Tuesday, 12 April 2016

Unknown

REAL MADRID ATAVUNJA UKUTA WA BERLIN LEO



Na Amini Nyaungo

Hukumu imezoeleka kutumika haswa mahakamani lakini pia katika michezo kuna watu wanatoa hukumu,Viktor Kassai Refaree kutoka  Hungary ndiye aliepewa Dhamana ya kutoa hukumu ya Mchezo mgumu wa marejeano kati ya Real Madrid dhidi ya Wolfsburg majira ya saa 9:45 usiku.

JE MADRID WATAWEZA KURUDISHA NA KUPITA?
Ni kazi ngumu sana haswa kwa mpira unaochezwa na Real Madrid kwa sasa lakini lolote linaweza kutokea hebu rudisha fikra zako msimu wa 2003-2004 wakati Arsenal tayari walisha fungwa Goli moja Highbury kabla ya kubadili matokeo pale Sansiro kwa kuwa funga Magoli 5 Inter Milan na Gunners ikapita hatua inayofuata lakini wakati huo Arsenal ilikuwa na watu kweli sio hawa waliopo sasa. kimtazamo Madrid anaweza kufanya mabadiliko ya kuwa funga zaidi ya Magoli yao lakini wakitaka salama wasikubali goli la mapema.

ZIDANE ANASEMAJE?
Ana uhakika kuwa matokeoa yanaweza kubadilika na wote wanao beza timu hiyo wasubiri dakika 90 zilizo baki

REKODI
Real Madrid ndio timu yenye mafanikio zaidi katika kombe hili wamechukua mara 10 na pia wana miliki kombe Halisi la michuano hiyo mara baada ya kulichukua mara tano mfululizo tangu lianzishwe 1954 hadi 1960 ndipo akakabidhiwa Kombe halisi la Uefa League.

Subscribe to Mtembezi Sports via Email :
Previous
Next Post »