Our Feeds

Sunday, 10 April 2016

Unknown

ISIHAKA HANA KINYONGO NA MAYANJA


Na Jacob Gamaly

NAHODHA msaidizi wa zamani wa Simba, Isihaka Hassan, amesema amerudi kundini akiwa hana kinyongo na kocha Jackson Mayanja na yupo tayari kwa ajili ya kuipigania timu yake kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.

Uongozi wa Simba ulimsimamisha kwa muda wa mwezi mmoja na kumvua cheo cha unahodha msaidizi kwa madai ya utovu wa nidhamu aliouonesha kwa Mayanja.

Isihaka anayeichezea Simba akitokea kikosi cha vijana cha timu hiyo, alisema mgogoro na kocha wake umechangia kuporomoka kwa kiwango chake kutokana na kuwa nje ya timu kwa muda ambao ulisababisha akose vitu vingi ambavyo wenzake walifundishwa.

“Kilichonitokea hadi kusimamishwa na uongozi ni kitu kibaya ambacho nisingependa mchezaji mwenzangu yeyote kimtokee, ukweli nilimkosea kocha, nimemuomba msamaha baada ya kulitambua kosa langu na sasa nimerudi kundini nikiwa sina kinyongo na kocha. “Lengo langu likiwa ni kushirikiana naye ili kuona namna gani tunaweza kuwa mabingwa msimu huu,” alisema Isihaka.

Beki huyo ambaye kwa sasa amenyoa rasta zake, alisema hivi sasa yupo tayari kumsikiliza na kufanya kila atakachoelekezwa na kocha huyo, akiamini ndiyo njia pekee ya kupata mafanikio.

Subscribe to Mtembezi Sports via Email :
Previous
Next Post »