Na Albogast Benjamin
Baada ya ligi kuu ya vodacom kusimama kwa muda kupisha michuano ya timu ya taifa pamoja na kuwepo kwa misukosuko kuhusu ratiba hiyo kuwa na viporo vingi husasani kwenye vilabu vya Yanga na Azam ambavyo vilikuwa na jukumu la kuwakilisha nchi kwenye michuano ya kimataifa sasa imerejea rasmi baada ya marekebisho kadhaa kufanyika.
Wikiendi hii kutakuwa na michezo 7 miwili ikichezwa leo jioni wakati michezo mingine mitano itapigwa siku ya kesho jumapili.
Moja ya mchezo utakao tazamwa zaidi ni mchezo utakaopigwa kwenye dimba la CCM Kirumba kati ya Toto African ya Mwanza dhidi ya Azam Fc kutokana na hali halisi ya msimamo ilivyo Azam wakiwa na nafsi ya kutwaa ubingwa hawatataka kupoteza ilihali Toto nao wakiwa na nia ya kushinda ili kujiweka kwenye mazingira salama ya kutoshuka daraja.
Mchezo mwingine ni wa Yanga na Kagera Sugar kwenye uwanja wa taifa, ni mechezo mhimu kwa timu zote Yanga akitaka kushinda ili kupunguza pointi kati yake na Simba lakini pia Kagera wanahitaji pointi tatu ili wahakikishe nafasi yao msimu ujao.
Ratiba kamili
Jumamosi
Mbeya City Vs Coastal Union
Mwadui Vs Mtibwa Sugar
Jumapili
Ndanda Vs Prisons
Ruvu Stars Vs African Sports
Stand United Vs Mgambo
Toto African Vs Azam
Young African Vs Kagera Sugar