Na Albogast Benjamin
Ni mchezo wa kipekee wenye historia ya aina yake, unakumbuka pale klop anaifunga Real Madrid kwenye nusu fainali na kufika fainali? Unakumbuka vizuri pale Wembley alivyofungwa na Bayern Munich kwenye mchezo wa fainali ya Uefa? Jinsi alivyozima ubabe wa Bayern Munich kwenye ligi ya Bundesliga? Hatimaye shujaa anarejea tena Iduna Park si mwingine ni Jurgen Klop akiwa na Liverpool kwenye michuano ya Ueropa.
Rekodi za timu hizi siku za hivi karibuni.
Mechi tatu za hivi karibuni Liverpool imeshinda mchezo mmoja,Dortmund imeshinda mchezo mmoja pia na zimetoka suluhu mchezo mmoja. kwa haraka haraka utagundua kitu kimoja tu hapo timu hizi zina ushindani mkubwa Liverpool alishinda 2 - 0 wakati Dortmund alishinda 2 - 1.
Kitu kikubwa kwa Klop.
Leo Klop anakutana na vijana wake aliowafundisha utamu wa soka na ukawaingia haswa nawazungumzia Marco Reus, Gundogan, Matis Hummels na wengine, Swali je Klop ataweza kuwazuia wasitumie mbinu alizowafundisha kumdhuru yeye na Liverpool yake?
Liverpool ya Klop ikoje?
Liverpool ni timu yenye historia yake kwenye mashindano ya kimataifa ambapo mara nyingi imekuwa ikifanya vizuri hata kama kwenye ligi haifanyi vizuri . Mwaka 2012 haikuwa vizuri kwenye ligi kiasi cha kutofuzu Uefa lakini ilifika fainali ya Europa na kufungwa na Atletico Madrid. Ikiwa na watu kama Coutinho, Lalana na Orig pamoja na kocha Jurgen Klop lolote linaweza tokea lakini kwa Dortmund yenye Aubameyang pia lolote linaweza tokea.
Pamoja na mechi hii kuna michezo mingine ya ligi ya Europa itakayopigwa usiku wa leo mechi zote zitachezwa saa tatu na dakika arobaini na tano kwa saa za Afrika mashariki.
Sporting Braga Vs Shakhtar Donetsk
Villarreal Vs Sparta Prague
Athletic Club Vs Sevilla San Mames
Borussia Dortmund Vs Liverpool