Our Feeds

Thursday, 7 April 2016

Unknown

MTEMBEZI THROWBACK: UNATAKA KUMJUA NWANKO KANU?

 
Na Amini&Albogast

Mtembezisports haiko nyuma kukuelezea masuala ya mpira na leo hii tuna kipengele kinaitwa MtembeziThrowBack (MTB).Tuna mchambua kwa ufupi mchezaji leo hii Tuta muangalia fundi Nwanko Kanu nahodha wa zamani wa timu ya Taifa ya Nigeria ambaye yupo Tanzania kwasasa na ametembelea taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete.

TUTATUMIA NAMBA KUELEZEA WASIFU WAKE.

Namba6. Idadi ya Vilabu alivyopitia kwenye maisha yake ya soka, wakati timu yake ya kwanza ilikuwa Iwuanyunwu Nationale

Namba25. Idadi ya michezo aliyoichezea timu yake ya kwanza ambayo ni Iwuanyunwu Nationale.

Namba 404. Hii ni michezo aliyocheza katika maisha yake ya mpira wa miguu akifunga jumla ya Magoli 98

Namba15. Idadi ya mabao aliyoifungua timu yake ya kwanza ya Iwuanyunwu Nationale.

Namba16. Amecheza timu ya Taifa miaka 16 kwa nidhamu kubwa

Namba30. Magoli aliyoifungia Arsenal kwenye michezo 119

Namba119. Ni idadi ya michezo aliyoicheza klabu ya Arsenal akipachika mabao 30. Mabao hayo yote amefunga akiingia kama mchezaji wa akiba.

Namba3. Ni mabao matatu aliyofunga kwenye mchezo wa Arsenal na Chelsea mchezo huo uliisha kwa Arsenal kushinda 3-2.

Namba25. Jezi aliyokuwa anavaa Arsenal kuanzia 1999-2004

Namba40. Hii ni miaka yake amezaliwa 1976

Namba49. Alikuwepo katika kikosi cha Arsenal kilicho cheza michezo 49 Bila ya kufungwa 2003-2004

Namba12. Ni idadi ya magoli aliyofunga timu ya Taifa kwa mechi 87

Namba1. Ni idadi ya Hat-Trick alizofunga akiwa na Arsenal na ilikuwa dhidi ya Chelsea. 

Subscribe to Mtembezi Sports via Email :
Previous
Next Post »