Our Feeds

Saturday, 9 April 2016

Unknown

KAMUSOKO NDANI,NIYONZIMA NJE DHIDI YA AL AHLY


Na Jacob Gamaly

Zikiwa zimesalia saa chache kuelekea mchezo wa mkondo wa kwanza hatua ya 3 ya mtoano kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika kati ya Dar es salaam Young African dhidi ya Al Ahly kwenye uwanja wa Taifa,tayari kikosi cha wanajangwani kimewekwa wazi.


Katika orodha hiyo kiungo na nahodha wa Timu ya Taifa ya Rwanda Haruna Niyonzima hakujumuishwa kutokana na kuwa majeruhi huku beki Mbuyu Twitte na Matheo Simon nao pia wakielezwa kuwa ni wagonjwa.

Kikosi kamili kitakachoanza leo.

Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul, Mwinyi Haji,Vicent Bossou, Kelvin Yondani, Thabani Kamusoko, Salum Telela, Simon Msuva, Deus Kaseke, Donald Ngoma na Amissi Tambwe.

Maneno ya Kocha wa Yanga.

Hans Pluijm ametanabaisha kuwa wamejizatiti kuhakikisha mchezo wa leo wanaibuka na ushindi huku wakiweka mkazo katika kuizuia Al Ahly wasipate goli la ugenini.

“Hii ni mechi ngumu tunacheza dhidi ya timu tunahitaji kuwaheshimu lakini sio kuwaogopa, tumefanya maandalizi lakini hii ni hatua moja mechi ni kitu tofauti na mazoezi, nafurahi kuona morali iko juu kwa vijana wangu sasa ni wakati wa kutafsiri tuliyoelekezana mazoezini kuja uwanjani,” amesema Pluijm.

Subscribe to Mtembezi Sports via Email :
Previous
Next Post »