Na Amini Nyaungo
Ndondo Cup jina hili limekaa ki-ukakasi kidogo lakini huku ndiko haswa mpira ulipo, wachezaji wengi Duniani wametokea kwenye Ndondo ingawaje nao wana jina lao. Kwa Tanzania hii ndio burudani kubwa sana vijana wengi huwa wana kusanyika wakinywa wakicheka wakivuta na hata vijana kutumia fursa kuuza bidhaa mbalimbali.
MCHEZAJI GANI MKUBWA AMETOKA KATIKA NDONDO
Alexis Sanchez moja ya jina kubwa Duniani nguzo ya Arsenal,anasifika kwa jitihada kukimbia hapa na pale,Kanu alisema kwa sasa mchezaji Bora wa Arsenal ni Sanchez. Huyu alitoka ndondo za nchini Chile hakutoka katika Academy tulizozoea kusikia wacheza wakubwa wenye kaliba yake wanatoka huko kwahiyo usiichukulie poa Ndondo ndio kiini cha mpira Duniani.
SPORTS EXTRA NDONDO CUP
Hawa wasichukuliwe poa wana fanya kitu kikubwa sana ambacho kina leta thamani ya vijana kuweza kupata ajira, 99% ya wachezaji wa kibongo huwa wanatoka katika Ndondo kwanini isipewe Thamani yake?
WAPI WAMEFELI?
Pamoja na jitihada kubwa hebu tujiulize maswali haya machache lengo si kuwaanzishia ili wapate ajira Maswali haya hapa:Kwanini Hawa tupi maendeleo ya wachezaji? kama wamepata timu mbona kuna vitu huwa wanatuambia mfano katika muziki? Lengo kujenga sio kubomoa isieleweke vibaya kazi wanayo ifanya ni kubwa mno kuweza kuwajumuisha watu kuwa katika sehemu moja sio rahisi.
PONGEZI
Hapa sasa waandaaji na wadhamini tuna wapongeza sana kwa tukio hili kubwa sio rahisi kuweza kujitolea na kutumia pesa pamoja na walioumiza vichwa kubuni kitu hiki, hongereni sana yaani ingewezekana hata mshindi atakae patika Ndondo akacheze michuano ya FA ili michuano hii ipate thamani.