Our Feeds

Saturday, 9 April 2016

Unknown

RAHA YA WIKIENDI LEO IPO HAPA


Na Amini Nyaungo

Msimu wa 2003/2004 ndio ulikuwa msimu mzuri kwa Arsenal kutokana na kilichofanyika wakati ule. Msimu huu kama Leicester wasingekuwa na roho ya Paka huenda furaha ya wananchi wa London Kaskazini yalipo makao makuu ya Arsenal ingerejea. Lakini nafasi bado ipo kama tu vikwazo kama hivi vya kukutana na West Ham atavivuka wakati huo akishinda msikitini na kukesha makanisani akiomba Mahrez augue Dengue ama Vardy ajikute anatatizo la Tezi dume.

Utamu wa Ligi ya England upo mchana huu pale Arsenal atakapo shushwa na treni ya mwendo kasi kwenye kitongoji cha WestHam na kuruhusu wabadilishe viatu na kuvaa daruga maalum kwaajili ya dakika 90 zenye umhimu wa pekee kwao mbele ya "LondonDerby" Usikose saa nane na dakika 45 mchana huu.

'SUPRISE' IPI LIGI YA ENGLAND MWAKA HUU

Kuanguka kwa  Timu kubwa msimu huu ndiko kuna ifanya Leicester City iwe 'SUPRISE'  hii imetokana na timu tulizo zoea kuingia Top Four kuangua mfano mzuri Manchester United,Liverpool na Chelsea Spurs na Leicester City  ingizo jipya katika Top four ya ligi hiyo.

MICHEZO YA LEO
Arsenal vs WestHam United 
Swansea vs  Chelsea
Manchester City vs Westbromwich Albion
Aston Villa vs Fc Bournemouth
Crystal Palace vs Norwich
Southampton vs Newcastle United
Watford vs Everton

JUMA PILI
Manchester United vs Tottenham spurs
Liverpool vs Stoke City


Subscribe to Mtembezi Sports via Email :
Previous
Next Post »