Wakati mwingine ukisubiri hadi walimwengu wakusifie huenda usizipate sifa zako bali uzianzishe mwenyewe huenda wakakuelewa au wakapokea tofauti. Mchezaji Ghali Duniani ambae amevunja rekodi ya kununuliwa £milioni 100 Garerh Bale ana haya ya kusema.
AMESEMAJE?
Bale ametanabaisha haya kupitia mtandao wa Uefa.com kuwa amefanya vizuri katika klabu ya Real Madrid tangu afike hapo pia amefanya yote aliyo takiwa kufanya. Bale amechukua Uefa mwaka huo aliofika wa 2013 alipofunga goli la ushindi dhidi ya Atletico Madrid pia tangu ajiunge hadi leo amechukua vikombe vinne, amecheza michezo 77 na kufunga magoli 43
MTAZAMO
Maswali ya kujiuliza je hayo anayosema ni kweli au dalili ya 'kufuria'? turudi nyuma Cristiano Ronaldo msimu aliofika 2009-2010 hakufanya vizuri kwa majeruhi na kuzoea ligi wakati huo alipewa jezi namba 9 akisubiri Raul ahame ili achukue jezi yake namba 7, hii ni dalili ya kushindwa kwa Bale ingawaje ameelezea vizuri jinsi alivyo fanikiwa.