Our Feeds

Monday, 11 April 2016

Unknown

SHIRIKISHO LA SOKA LA NIGERIA NFF LAWEKWA CHINI YA ULINZI WA POLISI

Kutoka Nigeria
Maafisa wa polisi wamezingira ofisi za shirikisho la kandanda la Nigeria NFF katika mji mkuu wa Abuja.
Maafisa wa kupambana na ghasia wakiwa wamevalia magwanda ya rasmi wamefunga afisi hiyo na hawamruhusu mtu yeyote kuingia ama hata kutoka ndani ya ofisi hizo.
Kauli hiyo inafatia uamuzi wa mahakama Alhamisi iliyopita uliompa madaraka Chris Giwa.
Mahakama ilitoa uamuzi kuwa Giwa alikuwa amemshinda mwenyekiti wa NFF Amaju Pinnick katika uchaguzi uliofanyika Septemba mwaka wa 2014.
Ijumaa iliyopita Giwa na washirika wake waliwasili katika ofisi hizo za NFF wakiwa wamejihami na uamuzi huo wa mahakama na wakaahidi kuanza kazi leo.
NFF imekata rufaa ya uamuzi huo ikidai kuwa Pinnick ndiye rais wa shirikisho hilo anayetambuliwa na shirikisho la soka duniani FIFA.
Haijulikani kwanini maafisa wa polisi wametumwa kulinda afisi hizo.
Wandani wa maswala ya kandanda hata hivyo wanatarajia Nigeria imepigwe marufuku ya muda na shirikisho la soka la dunia FIFA kwa kuingilia kati usimamizi wa kandanda.
Endapo FIFA itachukua hatua hiyo basi kampeini ya kufuzu kwa kombe la dunia itakuwa imetumbukia nyongo.
Crdt: BBCswahili

Subscribe to Mtembezi Sports via Email :
Previous
Next Post »