Na Albogast Benjamin
Kipa wa Arsenal Szczesny amekiri kuwa anatumai Leicester City itatwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza msimu huu na ndilo ombi lake
Szczesny anayechezea katika klabu ya Roma amekiri kuguswa na kikosi hicho cha Claudio Ranieri.
"Hakuna yeyote katika soka anayeweza kuelezea miujiza ya Leicester," aliiambia Sky Sports.
"Ingawa naiunga mkono Arsenal katika Ligi Kuu Uingereza, Ningependa kuiona timu ya Ranieri ikishinda." Aliongeza golikipa huyo aliyepo Roma kwa mkopo.
"Ni mfano wa kuigwa na hamasa kwa kila mmoja. Inasisimua kuwaangalia wakicheza." alimaliza