Our Feeds

Sunday, 10 April 2016

Unknown

LEICESTER CITY WAZICHUNGULIA MEDALI


Na Albogast Benjamin

Mchezo wa ligi kuu ya England uliomalizika jioni hii umezidi kutoa taswira ya nani anaelekea kuvaa medali kisha kunyanyua mikono isiyo mitupu bali mikono yenye taji la ligi.

Leicester City ikiwa kwenye mikono ya kocha mkongwe Claudio Ranieri ambaye amewahi kufanya kazi na vilabu vya Real Madrid na Ac Milan imezidi kujiweka kwenye mazingira ya kutwaa ubingwa mwaka huu baada ya kuwazawadia kipigo cha mabao 2 kwa 0 timu ya Sunderland kwenye uwanja wao wa nyumbani maarufu Stadium of Light.

Ni mshambuliaji Jamie Vardy ambaye kama hataugua mechi tatu zijazo basi nathubutu kusema kabati ama sebule za wachezaji kama Mahrez,Drinking water,Fuchs,Kante,Okazaki na wengine zitapambwa na medali majuma matatu yajayo na Historia itaandikwa.

Vardy ameweka kambani mabao yote mawili na kufanya wafikishe alama 72 kileleni baada ya kushuka dimbani mara 33. Tottenham wapo nafasi ya 2 wakiwa na michezo 32 jumala ya pointi 62 wakati The Gurners wakiwa na alama 59 baada ya michezo 32.

Subscribe to Mtembezi Sports via Email :
Previous
Next Post »