Na Amini Nyaungo
Wanasema historia zimewekwa ili zivunjwe wala si kingine, hivi ulishawahi kuona binadamu akamshika sharubu Simba au hata kushika mkia? ndio haswa msimu huu yanatokea huko England.
Jamhuri Kihwelo Julio huwa anasema KAMA POMBE YA SHUGHULI kila mmoja anachota anainywa hii imethibitika leo baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-0 ambacho kimeifanya Spurs kuzidi kuifukuzia Leicester City na kwa mara ya kwanza kwa miaka 15 Spurs wataweza kumaliza juu ya Arsenal.
MANCHESTER UNITED INAENDA WAPI
Kwa mwendo huu nayo pia inaweza kukosa nafasi nne za juu ambayo itampeleka akacheze Uefa Europa League kimsingi ligi hii ngumu sana.
Wakati huo huo Ujerumani Bundesliga Borrusia Dortmund inalegeza kamba baada ya kukubali sare ya mabao 2-2 kutoka kwa Schalke 04 hivyo kuachwa alama 7 mbele ya vinara Bayern Munich.