Our Feeds

Sunday, 3 April 2016

Unknown

VITA YA UBINGWA VPL SIMBA,YANGA NA AZAM HAIJAWAHI KUTOKEA





Na Albogast Benjamin

Kama kuna msimu ligi kuu ya vodacom ilishawahi kuwa tamu basi siamini kama inaweza kuuzidi msimu huu, maneno haya natamani yaeleweke ili uwe tayari kujua kwanini msimu huu ligi ni tamu kuliko misimu iliyopita?

Simba wakiwa kileleni na alama zao 57 wakiwa na michezo 24 wanahitaji ubingwa, wakati Yanga wakiwa nafasi ya pili na pointi zao 50 kwenye michezo 21 wanahitaji ubingwa pia, Azam wao wakiwa na alama 50 kwenye nafasi ya tatu wanahitaji ubingwa. Lakini kule chini JKT Ruvu ana pointi 21 kwenye nafsi ya 14 wakati African Sports yeye ana pointi 20 kwenye nafasi ya 15 na anayefunga mlango ni Coastal Union nafasi ya 16 akiwa na alama 19, ukichunguza vizuri kila timu hapo inanafasi ya kushuka au kubaki inatgemea na juhudi zake kwenye mechi za mwisho.


Hapa unaelewa nini?

Ni msimu wa kwanza kubaki mechi chache kama hizo wakati timu tatu zikiwa kwenye nafasi nzuri tu ya kutwaa ubingwa, tumezoea kuona Yanga na Simba au Yanga na Azam kwa miaka ya hivi karibuni zikibaki mechi tano basi unakuwa unaelewa nani anaweza kuwa bingwa au wawili wenye nafasi ya kuwa bingwa.

Mechi za leo kati ya Toto African na Azam Fc pamoja na ile ya Yanga dhidi ya Kagera Sugar ni vita isiyo na kikomo kutokana na uhalisia kwamba Azam anapambana na Simba na Yanga ili awe bingwa wakati Yanga anapambana na Azam na Simba ili awe bingwa hivyohivyo Simba anapamabana na Yanga na Azam ili awe bingwa ndio maana hapa nasema ligi ni taumu kuliko maelezo katika mechi hizi za mwisho.
Maana yake Timu hizi tatu zinapokutana na timu zingine hazifikirii kama ndio wapinzani wao ila wanafikiria zaidi nani anashindana nae pointi kuelekea ubingwa.

Subscribe to Mtembezi Sports via Email :
Previous
Next Post »