Na Albogast Benjamin
Ni katika kuutazama kwa jicho makini mchezo wa mkondo wa pili ligi ya mabingwa Ulaya hatua ya robo fanali baina ya Atletico Madrid na Barcelona mchezo utakaopigwa Vicente Calderon. Uefa imeamua kutumia kipengere cha uzoefu ili kumpata mwamzi atakayechezesha mechi hiyo yenye kila aina ya upinzani na ushindani.
Historia ya hivi karibuni inaonyesha kuibeba Barcelona kutokana na kushinda mechi zote 7 walizokutana hivi karibuni 4 zikiwa kwenye uwanja wa Camp Nou na tatu ni nyumbani kwa Atletico.
Uefa imemteua mwamuzi Nicola Rizzoli ambaye alichezesa fainali ya kombe la dunia 2014 nchini Brazil kati ya Argentina na Ujerumani na Messi atakuwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo huo, japokuwa msimu uliopita mwamuzi huyo huyo alichezesha nusu fainali ya Barcelona na Bayern Munich mkondo wa kwanza ambapo Barcelona walishinda mabao 3 kwa1.
Nicola mwenye miaka 44 ana uzoefu wa miaka 14 akichezesha ligi ya Seria A na michuano ya kimataifa na amepewa heshima hiyo ya kuamua nani aende nusu fainali kati ya Atletico na Barca Jumatano hii.