Na Amini Nyaungo
Msimu wa 2012-2013 Wigan Athletic wakati huo inafundishwa na kocha Robert Martnez ambae kwa sasa anaifundisha Everton kutoka pale England alifanya kama alicho kifanya Coast Union japo bado hajafika kileleni.
AMEFANYA NINI WIGAN ATHLETIC
Msimu huo Wigan iliingia fainali kwa bahati nzuri ikaifunga Manchester City na kunyanyua ubingwa wa FA nchini humo siku Tatu baadae akakutana na Arsenal na kufungwa ambapo safari ya kushuka daraja ikawahusu.
NINI KILICHO FANANA NA COASTAL UNION.
Nayeye amempiga mnyama na anaingia Nusu fainali ya FA huenda ikafika fainali pia kama akichukua ubingwa na akashuka daraja pia kwa msimamo ulivyo, timu zilizoingia hatua hiyo Azam,Coastal Union,Mwadui na Yanga
KIPI KIPYA MSIMU HUU
Kwa mara ya kwanza Azam two itaonesha upangaji wa tukio hilo Live leo mchana na hapo itaeleweka kabisa kuwa nani atakutana na nani wakati huo huo Kocha wa Mwadui Jamhuri Kihwelo anaomba akutane na Azam au Coastal huku akisubiri endapo Yanga ikichukua ubingwa timu yake ikiingia Fainali itaweza kuiwakilisha nchi hata kama ikifungwa.