Our Feeds

Friday, 1 April 2016

Unknown

TFF HALI MBAYA YAPIGA MAGOTI WIZARANI


NA MWANDISHI WETU, Dar


HALI si hali ndani ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), baada ya leo asubuhi Katibu Mkuu wa shirikisho hilo Mwesigwa Celestine, kufunga safari kwenda kwa Wizara ya Habari, Tamaduni, Sanaa na Michezo, kujadili kuhusu deni la Sh. Bilioni 1.600, wanalodawiwa na Mamlaka ya Mapato nchini TRA.

Katikati ya wiki mabasi matano ya TFF, yalikamatwa na na Madalalai wa Mahakama (Yono Auction Mark) na TFF, kutakiwa kulipa deni hilo lililoanza tangu mwaka 2010 mpaka 2015.

Akizungumza na Simba Makini, mmoja ya watendaji wa TFF, aliyekataa kutajwa jina lake alisema, hali ni mbaya na Katibu ameenda Wizarani kuzungumza ili aone kitu gani kinaweza kufanyika.

Mtendaji huyo alisema, licha ya Rais wa sasa wa TFF, (Jamal Malinzi) kuwa na dhamana ya deni hilo, lakini ‘amepigishwa shoti’ na kiongozi aliyepita.

“Asubuhi hii Katibu alituambia hali ni mbaya na anaenda Wizarani kujua nini hatima ya TFF na mabasi ambayo yamechukuliwa.

“Si kizu kizuri ambacho kimo humu ndani (TFF), lakini jamaa (Malinzi) hiki si kimeo chake, lakini yeye ndio kiongozi anayeshikilia hivi sasa, hivyo ni lazima abebe huo msalaba. Maana katika deni hilo kuna majumuisho ya mchezo wa Tanzania na Brazil mwaka 2010, muda ambao Malinzi hakuwa madarakani, lakini ndio hivyo wacha tuone nini mwisho wake” alisema mtu huyo.

Subscribe to Mtembezi Sports via Email :
Previous
Next Post »