Our Feeds

Saturday, 9 April 2016

Unknown

SAMATTA AZIDI KUPASUA ANGA

Samatta

Na Amin Nyaungo

"Nilikuwa natoka nyumbani saa 11 Alfajiri Nafika uwanjani nalala wakati nina cheza Simba, Patrick Phiri aliniuliza kwanini kila siku nakukuta uwanjani? nikamueleza kuwa nataka kufika mbali ikafika siku akanambia kuwa nitapata mafanikio" maneno ya MBWANA SAMATTA katika moja ya mahojiano yake na SportsBar ya ClousdTv.

Kujitunza na heshima kutilia mkazo kile unacho kifanya, kiongozi Mmoja aliwahi kutumka kuwa kama wewe mwandishi basi andika sana kama unafanya Burudani(intertainment) fanya sana , alikuwa na maana kubwa sana na hii inaonekana kwa kijana wa Tanzania Mbwana Ally Samatta ambae anacheza mpira wa kulipwa Nchini Ubelgiji japo ligi yao ina mzunguko usio eleweka lakini kijana wetu anang'ara.

MALENGO 

Mbwana Samatta mara zote anawaza kucheza ligi kubwa haswa England alishawahi kusema kwa mwenendo huu lazima afike na atafika kwa uwezo wa Mungu, Mrisho Ngassa alishangaa mji pale London alipo enda kujaribu Westham United pia alishangaa mchezaji kula kuku mzima wakati yeye hata nusu hamalizi lakini Samatta anaweza kuendana na yote na kutia kamba kila siku.

MAFANIKIO

Hana mafanikio makubwa lakini ndani ya  timu huwa wanasema ni mtu mchangamfu na mkiwa katika vyumba vya kubadilishia nguo huwa lazima mcheke, hii aliiweza Lukas Podolsk wakati yupo Arsenal sio wote wanae weza kuwafurahisha wachezaji wenzao,Samatta amefunga magoli 3 hadi sasa mawili akitokea kama mchezaji wa hakiba na moja akianza katika kikosi cha kwanza.

MATOKEO YA GENK NA MTAZAMO

Fc Genk imepata ushindi wa mabao 4-0 Mbwana akaingia Dakika ya 76 na ana vaa namba 77 kafunga goli dakika ya 77 , msimu unao fuata baada ya msimu huu huenda tukasikia ofa mbali mbali kutoka vilabu vya England na Spain hawa huwa ndio wanunuzi wakuu wa wachezaji wa Genk.

KILA LA KHERI SAMATTA.

Subscribe to Mtembezi Sports via Email :
Previous
Next Post »