Na Albogast Benjamin
Boss wa Manchester City Manuel Pellegrini amewataka wachezaji wake kusonga mbele bila kuchoka hadi watakapochukua ubingwa wa ligi ya mabingwa Ulaya Uefa.
Manchester City imefuzu hatua ya nusu fainali kwa mara ya kwanza baada ya kuwatoa mabingwa wa Ufaransa Paris St Germain kwa jumla ya mabao matatu kwa mawili.
Pellegrini alijibu baada ya kuulizwa swali na waandishi wa habari kwenye uwanja wa Etihad kama atashinda Uefa msimu huu alijibu kwa kujiamini alisema "lazima tuchukue maana ni moja ya mipango inayotakiwa ikamilike kutokana na uwekezaji mkubwa"
"Tumekuwa tukikosolewa kwa mengi sana lakini nina uhakika kiwango cha timu kinapanda kila siku na moja ya mipango ya klabu hii ni kuchukua Uefa hivyo hilo likitimia kila kitu kitakuwa sawa japo haimanishi ndio utakuwa mwisho wa mipango mipya." Alimaliza Pellegrini.