Na Albogast Benjamin
Mmiliki wa timu ya Leicester City Vichai Srivaddhanaprabha inayoshiriki ligi kuu ya soka ya Engaland maarufu kama EPL ametoa zawadi ya chupa moja ya bia au maji pamoja na Donati moja kwa kila shabiki wa timu hiyo aliyekuwa na tiketi ya mchezo wa leo dhidi ya Southampton.
Boss huyo ametoa zawadi hiyo kwa mashabiki kama sehemu ya kusheherekea siku yake ya kuzaliwa ambayo ni kesho jumatatu lakini ameamua kufanya hivyo leo kutokana na timu hiyo kuwa na mchezo wa nyumbani kwenye dimba lake la Kings Power ikiwakaribisha Southampton.
Vichai Srivaddhanaprabha amewashukuru mashabiki wa timu hiyo kwa kuwa pamoja na timu yao tangu mwanzo wa msimu hadi ilipofika sasa.
Mkurugenzi wa timu hiyo Susan Whelan amesema kuwa boss Srivaddhanaprabha amekuja nchini Uingereza kwaajili ya kuipa nguvu timu yake kwenye kipindi hiki cha mechi za mwisho wakiwa moja ya vilabu vyenye nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa msimu huu.
Mr. Srivaddhanaprabha atarejea nchini kwake Thailand mara baada ya mchezo wa leo ambao unaendelea hivi sasa na Leicester City wanaongoza kwa bao moja kwa sifuri dhidi ya Southampton bao limefungwa na Wes Morgan dakika ya 38.
Leicester City wanaongoza kwa ligi wakiwa na alama 66 hadi sasa.