Our Feeds

Sunday, 3 April 2016

Unknown

WAHUSIKA WA UPANGAJI MATOKEO LIGI DARAJA LA KWANZA WABAINIKA NA HIZI NI ADHABU WALIZOPATA



Na Amini Nyaungo

Ripoti ya kamati ya Tff iliyosomwa na wakili wa kujitegemea Jerome Joseph imebaini makosa mbalimbali kwenye Ligi Daraja la kwanza iliyomalizika mapema mwaka huu na kukumbwa na sakata la upangaji matokeo kwenye mechi mbili za mwisho kundi C zilizokuwa na maamuzi ya nani apande ligi kuu ambapo Rungu la Tff limeamua haya yafuatayo kwa kundi C.

Timu zote zilizo shiriki kundi C zimeshushwa Daraja zitacheza ligi Daraja la kwanza wakati Fc Kanembwa imerudishwa kucheza Ligi ya mkoa.

Na hii ndio ripoti kamili.


1.Refa wa mchezo Kanembwa na Geita Akafungiwa maisha kujihusisha na mpira


2.Kamisaa wa mchezo huo naye akafungiwa maisha

3.Kocha Msaidizi wa Geita naye kafungiwa maisha

4.Kipa Kanembwa kafungiwa miaka 10 na faini milioni 10

5.Kipa Geita anafungiwa miaka 10 faini milioni 10

6.Katibu wa Chama cha mpira Tabora kafungiwa maisha.

7.Kipa ni Denis aliwahi kucheza Simba B

8.Refa Mkeremi kati ya Polisi na Oljoro kafungiwa miaka 10, faini milioni 10

9.Hamisi Machunde 4 Refalii kafungiwa miaka 10

10.Kocha msaidizi Polisi Tabora kafungiwa maisha

11.Mwenyekiti Oljoro kafungiwa maisha.

12.Mwenyekiti wa Chama cha mpira Tabora Bw. Kitumbo kafungiwa maisha!

13.Geita na Kanembwa zimeshushwa Daraja. Kanembwa Ligi ya Mkoa Geita Daraja la pili

14.Polisi Tabora na Oljoro zimeshushwa Daraja hadi Daraja la pili.

Subscribe to Mtembezi Sports via Email :
Previous
Next Post »