Kutoka kushoto ni msemaji wa TADA,Katikati ni Makamo M/kiti TADA na Kulia ni Katibu mkuu wa TADA |
Na Moshi Shabaan
Chama cha Mchezo wa Vishale Tanzania (TADA) kinatarajia kufanya shindano la wazi la kimataifa la shirikisho la mchezo wa vishale Afrika Mashariki litakaloanza April 29 hadi Mei 1.
Shindano hilo litafanyika jijini Dar es salaam eneo la Moshi Hotel na litashirikisha nchi wanachama za Kenya, Uganda na Rwanda.
Katibu Mkuu wa Chama hicho Subira Waziri amesema kuwa Tanzania ni nchi mwanachama wa shirikisho la mchezo huu wa vishale la Afrika Mashariki lijulikanalo kama (East Africa Darts Federation) hivyo kutokana na utaratibu wa uandaaji wa mashindano mwaka huu Tanzania ndio itakua wenyeji wa shindano hili.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Darts Tanzania Bi Redempta Mwebesa amesema kuwa mchezo huu kwa kusikia tu huwezi kuelewa maana na uchezaji wake hivyo kuwaomba wananchi wajitokeze kwa wingi kuangalia mchezo huu, vilevile zawadi za washindi wanategemea kutumia vikombe vya zamani na pesa taslim za viingilio hivyo kuomba wadau wote wa michezo ndani na nje ya nchi kujitoa kwa hali na mali ili kuendeleza mchezo huu nchini.