Na Albogast Benjamin
JOSEP GUARDIOLA SALA jina maarufu sana duniani kwa wapenzi wa soka duniani kote amepata umarufu akiwa mchezaji ndani ya Barcelona na baadae kuwa kocha wa timu hiyo
Barcelona ndiyo haswa iliyompa jina kubwa duniani kote hata walioanza kushabikia mpira miaka ya karibuni wakawa wana muelewa kwa mafanikio aliyoyapata kwa muda mfupi aliofundisha Barcelona
18 January 1971 ndio mwaka ambao amezaliwa Pep lakini maisha ya soka yalianza mwaka 1984 akiwa ndani ya kituo cha michezo cha Barcelona maarufu kama La Masia na mwaka 1990 ndio alipata namba kwenye timu ya wakubwa na hapo ndio historia ya utawala wa soka kwake ilianza.
Maisha ya ukocha
Pep rasmi aliiingia kwenye ukocha mwaka 2007 akiwa na Barcelona B iliyokuwa na nyota kama Fabregas,Busquet,Messi na Pedro na mwaka 2008 alitangazwa Rasmi kuwa kocha mkuu wa Barcelona na alitengeneza timu ya ushindi akiwatoa watu kama Ronaldinho na Et'oo akiwapa nafasi kina Messi na wengine ambao walimsadia kutwaa makombe 4 ya La liga na mawili ya Uefa pamoja na makombe mengine kama Kombe la mfame na Klbau bingwa ya dunia.
Mwaka 2012 aliamua kupumzika lakini mwaka 2013 aliibukia Bayern ambako amefanikiwa kubadili mfumo mzima wa uchezaji wa timu ya Bayern na kuwafanya wacheze mpira wa pasi nyingi kiasi cha kuwa timu iliyomiliki mpira kwa asilimia nyingi kwa misimu miwili ya 2014 na 2015.
Usikose sehemu ya pili tutazame ujio wake kwenye ligi ya Uingereza.