Our Feeds

Saturday, 9 April 2016

Unknown

UEFA KUZIWAJIBISHA LIVERPOOL NA DORTMUND


Na Albogast Benjamin

Mwezi October mwaka 2013 kwenye mchezo wa Simba na Kagera uwanja wa taifa mashabiki wa Simba walivunja viti takribani 100 baada ya kutoridhishwa na maamuzi ya mwamuzi Mohamed Theofile na timu ya Simba ilikumbwa na adhabu kutoka TFF na ililazimika kutoa gharama za matengenezo.

April 8 mwaka huu ulifanyika mchezo wa robo fainali ya michuano ya Europa kati ya Borrusia Dortmund na Liverpool kwenye uwanja wa Signal Iduna Park mjini Dortmund.

Shirikisho la soka barani Ulaya Uefa linazichunguza klabu za Borussia Dortmund na Liverpool  kutokana na mashabiki wake kuonesha utovu wa nidhamu kwenye mchezo wao ambapo mashabiki wa Liverpool wanatuhumiwa kwa kurusha baruti wakati wa kushangilia bao la Origi.

Mashabiki wa Dortmund wanatuhumiwa kwa kuvunja uzio wa ndani ya uwanja na kama watakutwa na hatia watapata adhabu kama ambayo walipata Simba japo itatofautiana thamani na gharama.

Subscribe to Mtembezi Sports via Email :
Previous
Next Post »