Our Feeds

Wednesday, 13 April 2016

Unknown

TUZO YA MCHEZAJI BORA EPL NI VITA YA HARRY KANE,VARDY,OZIL NA MAHREZ


Na Amini Nyaungo

Edin Hazard ndie mmliki wa Tuzo ya Mchezaji bora wa Mwaka wa England ambayo iliipata msimu uliopita na mchezaji chipukizi amechukua Harry Kane kama una fuatilia mpira mwaka huu yamerudi tena nani nani wameingia katika kinyang'anyiro hiko?

MCHEZAJI BORA WA MWAKA ENGLAND (PFA)
Harry Kane amechaguliwa katika vipengele viwili mchezaji bora wa Mwaka na mchezaji Bora kijana huyu anatokea Tottenham Spurs. 

Mesut Ozil naye ameingia katika kogombania mchezaji bora wa mwaka hii ilitokana na usaidizi wake wa kupatikana kwa mabao (Assist) amesaidi 18 zimebaki mbili aifikie Rekodi ya Thiery Henry.

Wengine wanao Gombania uchezaji Bora wa mwaka ni

N'golo Kante
Dimitr Payet
Jamie Vardy
Riyad Mahrez

Wakati wachezaji vijana wamechaguliwa
Dele Alli
Harry Kane
Jack Butland
Phillipe Coutinho
Romelu Lukaku
Ross Barkley

Washindi mara 8 katika misimu 11 iliyopita wametoka Manchester United Liverpool na Chelsea.

Unknown

SHINDANO LA WAZI LA DARTS KUFANYIKA DAR

Kutoka kushoto ni msemaji wa TADA,Katikati ni Makamo M/kiti TADA na Kulia ni Katibu mkuu wa TADA


Na Moshi Shabaan 

Chama cha Mchezo wa Vishale Tanzania (TADA) kinatarajia kufanya shindano la wazi la kimataifa la shirikisho la mchezo wa vishale Afrika Mashariki litakaloanza April 29 hadi Mei 1.

Shindano hilo litafanyika jijini Dar es salaam eneo la Moshi Hotel na litashirikisha nchi wanachama za Kenya, Uganda na Rwanda. 

Katibu Mkuu wa Chama hicho Subira Waziri amesema kuwa Tanzania ni nchi mwanachama wa shirikisho la mchezo huu wa vishale la Afrika Mashariki lijulikanalo kama (East Africa Darts Federation) hivyo kutokana na utaratibu wa uandaaji wa mashindano mwaka huu Tanzania ndio itakua wenyeji wa shindano hili.
 
Naye Makamu Mwenyekiti wa Darts Tanzania Bi Redempta Mwebesa amesema kuwa mchezo huu kwa kusikia tu huwezi kuelewa maana na uchezaji wake hivyo kuwaomba wananchi wajitokeze kwa wingi kuangalia mchezo huu, vilevile zawadi za washindi wanategemea kutumia vikombe vya zamani na pesa taslim za viingilio hivyo kuomba wadau wote wa michezo ndani na nje ya nchi kujitoa kwa hali na mali ili kuendeleza mchezo huu nchini.
Unknown

ROBO FAINALI UEFA LEO NI MWENDO WA KAMPA KAMPA TENA


Na Albogast Benjamin 

Ifikapo saa tatu na dakika arobaini na tano usiku 9:45, utakuwa ni muda wa wapenda soka kuelekeza macho yao pale kwenye dimba la Vicente Calderon nyumbani kwa Atletico Madrid, kwenye mchezo wa robo fainali mkondo wa pili ambayo ni kumbukumbu tosha ya msimu wa 2014 ambapo Barcelona waliaga katika hatua hiyo na kuwaacha Atletico wakitinga hadi hatua ya fainali.

Vikosi vya msimu huo:

Atlético:  Courtois, Juanfran, Godín, Miranda, Filipe Luís, Gabi, Tiago, Koke, Adrián López (Diego 62), Raúl García, Villa (Rodríguez 79).
Barcelona:  Pinto, Alves, Bartra, Mascherano, Alba, Xavi, Busquets, Iniesta (Pedro 72), Fàbregas (Alexis Sánchez 61), Messi, Neymar.
Mchezo huo uliamuliwa na goli pekee la Koke dakika ya 50 na kuharibu rekodi ya Barcelona ya kufika nusu fainali misimu sita mfululizo.

Mchezo wa leo:
Wiki moja iliyopita timu hizi zilicheza pale Camp Nou na matokeo yalikuwa ni 2 kwa Barca na 1 kwa Atletico, Mchezo wa leo unategemewa kuwa na ushindani wa hali ya juu ambapo kila timu inayo nafasi ya kusonga mbele ukizingatia Atletico wanahitaji bao moja tu huku Barcelona wakitafuta sare yoyote ili wasonge mbele. Mwamuzi Nicola Rizzoli ndiye ataamua dakika 90 za pambano hilo.


Mchezo mwingine:

Mchezo mwingine usiku wa leo utapigwa nchini ureno kati ya Benfica  na Bayern baada ya mchezo wa kwanza uliofanyika Alianz Arena kumalizika kwa Bayern kushinda bao moja. Benfica ambayo inaonekana kurejea kwenye ubora wake kama ule wa mwaka 2006 ilipokutana na Barcelona kwenye robo fainali itakuwa inasaka tiketi ya nusu fainali mbele ya kikosi cha Bayern ambacho kinafundishwa na kocha Pep Guardiola na ndoto yake kubwa ni kubeba taji hili kabla hajatua Manchester City msimu ujao.
Unknown

BOSS WA SOKA LA ZANZIBAR KUPATIKANA KESHO



Na Martha Magawa

Kinyang'anyiro cha kuwania nafasi tatu za juu za Chama Cha Soka Zanzibar ZFA, kitajulikana baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa chama hicho, uchaguzi huo utakaofanyika kesho saa nne za asubuhi katika uwanja wa Gombani, huku ukiwa chini ya ulinzi mkali wa askari Polisi, Mgeni Rasmi akitarajiwa kuwa Mkuu wa wilaya ya Chake Chake Mhe:Hanuna Ibrahim Masoud.

Uchaguzi huo ambao wajumbe 60 wa mkutano mkuu wa ZFA Zanzibar, wataweza kuchagua Rais na makamo wake wawili ambao ndio watendaji
wakuu wa Chama hicho.

Jumla ya wagombea wawili wameweza kujitokeza katika kuwania nafasi hiyo ya uras akiwemo Rais aliyepo Madarakani, Ravia Idarous Faina, huku akikabiliwa na upinzania mkali kutoka kwa Kocha Salum Bausi.

Nafasi ya Makamo wa Rais wa ZFA Taifa Pemba Ali Mohamed Ali akichuwana na Suwedi Hamad Makame, huku Upande wa Uguja wanaogombania nafasi ya Makamo ambayo imewachwa wazi na Haji Ameir Haji, aliyevuliwa nafasi hiyo na wajumbe wa mkutano mkuu wa ZFA, ikigombaniwa na Mohamed Massoud Rashid, Ali Salum Nassor na Mzee Zam Ali.

Akizungumza mtembezi juu ya maandalizi ya Uchaguzi huo Makamo wa ZFA Taifa Pemba Ali Mohamed Ali, alisema maandalaizi yote ya Uchaguzi huo yameshakamilika, ikiwemo kwa wajumbe kutoka unguja kuwasili Pemba pamoja na waandishi wa habari za michezo Unguja.
Unknown

LUIS ENRIQUE: BARCELONA NI BORA



Na Amini Nyaungo

Kuwapa Nguvu na hamasa wachezaji ni moja ya kazi kubwa ya kocha wa mpira wa miguu na kiongozi yoyote William Gallas alivuliwa unahodha na kupewa Cesc Fabrigas kwa kukosa utulivu wa uongozi.

Gallas alishindwa kuzuia hisia zake mara baada ya kufungwa badala yeye ndio awatulize wenzake akaanza kulia yeye badala ya kutuliza wenzake,na Fabrigas akapewa beji hiyo kubwa japo umri  ulikiwa mdogo.Ferguson alikuwa ana wafokea wachezaji katika vyumba vya kubadilishia nguo baada ya kipindi cha kwanza.

Kocha bora wa Dunia Luis Enrique amewaweka sawa wachezaji wake mara baada kupoteza Michezo miwili katika ligi na kuweka Rehani Ubingwa wa La liga, leo wana kutana na Atletico Madrid Vicente Caldelon.

"Tunataka tuwaoneshe watu kuwa Barcelona ni bora kwenye mchezo na Atletico Madrid" maneno ya Enrique alipokuwa akiongea na waandishi juu ya mchezo wao.

Manufaa ya kauli hii.

Kauli hii kama ya kujihami baada ya kupoteza katika ligi na ugumu wa mchezo wa leo wa Ligi ya Mabingwa kauli hiyo itaweza kuwa na Manufaa kwa wachezaji wake na Benchi zima la ufundi la timu hiyo.

Unknown

PELLEGRINI: MAN CITY TUTACHUKUA UBINGWA MSIMU HUU


Na Albogast Benjamin

Boss wa Manchester City Manuel Pellegrini amewataka wachezaji wake kusonga mbele bila kuchoka hadi watakapochukua ubingwa wa ligi ya mabingwa Ulaya Uefa.

Manchester City imefuzu hatua ya nusu fainali kwa mara ya kwanza baada ya kuwatoa mabingwa wa Ufaransa Paris St Germain kwa jumla ya mabao matatu kwa mawili.

Pellegrini alijibu baada ya kuulizwa swali na waandishi wa habari kwenye uwanja wa Etihad kama atashinda Uefa msimu huu alijibu kwa kujiamini alisema "lazima tuchukue maana ni moja ya mipango inayotakiwa ikamilike kutokana na uwekezaji mkubwa"

"Tumekuwa tukikosolewa kwa mengi sana lakini nina uhakika kiwango cha timu kinapanda kila siku na moja ya mipango ya klabu hii ni kuchukua Uefa hivyo hilo likitimia kila kitu kitakuwa sawa japo haimanishi ndio utakuwa mwisho wa mipango mipya." Alimaliza Pellegrini.

Unknown

ARTETA NA GUARDIOLA HUENDA WAKAKAA BENCHI MOJA



Na Amini Nyaungo

Kuna maisha baada ya kucheza mpira mifano mizuri ipo hata hapa Tanzania japo sio wote wanao fikiria maisha baada ya uchezaji, nenda kamulize Msuva ana lengo gani baada ya kustaafu mpira sijui atakwambia nini? 

Mikel Arteta kukaa benchi moja na Pep Man City
Kiungo na Kapteni wa Arsenal Mikel Arteta imearifiwa na ESPN kuwa mchezaji huyu atajiunga na Manchester City katika Benchi la ufundi ili kutoa huduma katika benchi la ufundi wa timu hiyo.

Guardiola wanamahusiano gani?
Walikutana pale La masia katika Academy ya Barcelona kabla Mikel Arteta kutimka na walikuwa marafiki sana sasa taafira zinasema kuwa Gurdiola anataka kumsogeza Manchester City kutokana na uzoefu wa ligi hiyo.

Arteta ni nani?
Kiungo bora kabisa haswa alipata umaarufu akiwa Everton alicheza vizuri alisajiliwa na Arsenal baada ya kufungwa magoli 8-2 dhidi ya Manchester United 2011 maisha yake Emirate haya kuwa Mazuri sana baada ya kuandamwa na Majeruhi ya mara kwa mara kama ilivyokuwa kwa winga wa Simba Uhuru Suleiman.

Alijiandaa kwa hili?
Baada ya kuona maisha ya uchezaji yanaenda kombo ameamua kusomeshwa na timu hiyo ili afundishe Kikosi cha pili  cha Arsenal na Tayari amepata vyeti hivyo itakuwa Rahisi kuwa kocha. Na huu ndio msimu wake wa mwisho Arsenal kwa mwendo wake wa Majeruhi.